SWAHILI

Mshauri ni mtu ambaye unamheshimu na yupo katika nafasi ya kutoa ushauri na mwongozo katika elimu yako au kazi yako. Kutafuta mshauri mzuri inaweza kuwa jambo gumu sana.

Sifa za mshauri mwema ni:-

Muda – Kama hana muda  hawezi kukusaidia vizuri au hata kukupa ushauri tu.

Wingi wa maarifa – madumuni ya kuwa na mshauri ni kukusaidia wewe katika matatizo unayokutana nayo  katika maisha, na si tu matatizo unayopata katika elimu au kazini kwako. Hiyov mtu mwenye maarifa ukimpata ufurahi sana.

Moyo mzuri – kuna mambo mengi katika dunia hii ambayo ni unethical kwa kufanya, lakini bado kisheria ni halali kufanya. Unataka mtu na maadili mema ili kukusaidia au mwingine anaweza kukushauri kufanya mambo unethical.

Nia ya kukupa ujuzi na maarifa aliyonayo –  Kama mshauri wako ni mwenye ujuzi sana lakini si tayari kukusaidia yeye hayuko tayaku kuwa mshauri wako.

Mwenye shauku ya mambo au field unayosoma au kama ni kazi unayofanya.

Mwenye kuonyesha matendo mazuri na mifano ya kuiga.

Mwenye kudhamini kujifunza kila mara nakuwa elimu haiishii darasani tu na mtu ambaye anapenda kulenga juu katika maendeleo.

Mtu anayefurahia mafanikio yako.

Mtu anayetoa ushauri na maoni ya kukujenga.

Baada ya kupata mtu ambaye unamwona ni mshauri mzuri jambo lakufanya ili aweze kukusaidia vizuri ni:-

Mheshimu – Mtu hawezi kukusaidia kama humuheshimu.

Jitahidi uwe rafiki yake mzuri – Kabla ya kuanza kumuuliza mtu na kumweleza mtu matatizo yako, au kutegemea akushauri mambo yako, ni lazima kupata kumjua vizuri. hakunamtu atakaye anza kukushauri au kukukosoa kama hakufahamu vizuri.

Kuwa mkweli katika matarajio yako – Kuwa na mshauri sio kuw aitakubadilisha maisha yako, kazi yako au elimu yako kwa usiku mmoja. Inategemea juhudi zako pia na kuongezea ushauri unaopewa.

Tafadhali Zingatia: Sisi hapa tupo ili kukusaidia kuungana na mtu tunayefikiria atakua mshauri wako mzuri kutokana na form zinazojazwa hapa kwenye blog yetu.  Hatuwezi kuthibitisha matokeo ya mwisho. Kama kwa sababu fulani unafikiri mshauri uliyempata halingani na matarajio yako, ni heri kuwa mkweli na kuanza kutafuta mshauri mwingine. Ila sio uanze kuonyesha dharau kumbula mtu anayekusaidia ni kutokana na moyo wake.  Ila usisahau na wewe kutafuta mtu au watu wa kuwapa ushauri huwezi jua unachokifahamu kitamsaidiaje mtu mwingine.

Leave a comment